Ripoti YA safari ya SKAUTI NCHINI KENYA
iliyofanyika tarehe hadi tarehe 9/9 mpaka tarehe 14/9/2018
UTANGULIZI
Safari hii ya siku 5 ilihusisha vijana wa skauti wa shule ya
sekondar iKaloleni, shule ya msingi Safina na shule ya msingi Mother Kelvin wapatao 28 ikiwa na viongozi 05. Viongozi
wa kike wakiwa 03 na wakiume wa kiwa 02.
Safari hii ilianzia Boma saa
1.30 asubuhi na kisha njia panda saa 5.00 asubuhi kwaajili ya kuwachukua
vijana na viongozi wa shule ya msingi Mother Kelvin ya Same. Safari ikaanza rasmi. Vijana hawa na viongozi
wakaanza rasmi safari yao kwa kupitia njia yaTarakea mpaka Nairobi- Kenya.
Madhumuni ya
Safari
Lengo la safari
hii lilikuwa ni:-
1.Kuimarisha
mahusiano yaliyopo kati ya skauti wa nchini Kenya na Tanzania.
2.Kubadilishana
uzoefu kati ya skauti wa nchini Kenya na Watanzania.
3.Kujifunza
mbinu mbalimbali za kiskauti
4.Kutembelea
eneo alilozikiwa muanzilishi wa skauti
5.Kutembelea
eneo alilokuwa anaishi mwanzilishi wa skauti nchini Kenya.
6.Kufanya
utalii katika maeneo mbalimbali ya nchini Kenya.
Mahudhurio